B asi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Wakolosai 3:1 Ninakukaribisha tena kwa imani,twende tujifunze pamoja neno la uzima.Kwani ni nguvu na ni afya yetu ya kiroho. Na kristo atuwezeshe kupitia Roho mtakatifu amina. M singi wa fundisho la leo ni ? YAFUATENI AU YAPANIENI YALIYO JUU. K atika somo lililopita tulijifunza kuweka nia au lengo kabla ya kutenda,na leo tutaona kufuata au kupania. BASI YAFUATENI¡¡}》》》》》 N eno hili tukiliangalia kwa undani lina maana kubwa sana ni kama kusema,tazameni,shikilieni,fuateni,ishini au YAF...
WAGALATIA 5:16 "Basi nasema.Enendeni kwa Roho,wala hamtazitiza kamwe tamaa za mwili. K atika barua ya Paulo kwa Wagalatia 5:16, anasema hivi: "Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili." K atika muktadha huu, Paulo anatuhimiza Waamini kuishi maisha yanayoongozwa na Roho Mtakatifu badala ya kushughulikia na kuridhisha tamaa za mwili. Katika maandiko ya Paulo, "Roho" inamaanisha Roho Mtakatifu ambaye anakuja kuishi ndani yetu wakati tunapo pokea wokovu kwa imani katika Kristo. Kuishi kwa Roho kunahusisha kuwa na uhusiano mzuri na Mungu kupitia kuunganika na Roho Mtakatifu. Kuongozwa na Roho Mtakatifu kunamaanisha kufuata mwongozo wa Mungu, kudumisha tabia na matendo yanayoambatana na ukweli na haki, na kuepuka kutenda tamaa za mwili ambazo haziendani na mapenzi ya Mungu. Wagalatia 5:22-23: "Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakun...