Skip to main content

Posts

"YAFUATENI YALIYO JUU KRISTO ALIKO"

B asi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Wakolosai 3:1 Ninakukaribisha tena kwa imani,twende tujifunze pamoja neno la uzima.Kwani ni nguvu na ni afya yetu ya kiroho. Na kristo atuwezeshe kupitia Roho  mtakatifu   amina. M singi wa fundisho la leo ni ?                                                         YAFUATENI AU YAPANIENI YALIYO JUU. K atika somo lililopita tulijifunza kuweka nia au lengo kabla ya kutenda,na leo tutaona kufuata au kupania.  BASI YAFUATENI¡¡}》》》》》                                                     N eno hili tukiliangalia kwa undani lina maana kubwa sana ni kama kusema,tazameni,shikilieni,fuateni,ishini au YAF...
Recent posts

''ENENDENI KWA ROHO KAMWE HAMTAZITIMIZA TAMAA ZA MWILI''

      WAGALATIA 5:16 "Basi nasema.Enendeni kwa Roho,wala hamtazitiza kamwe tamaa za mwili. K atika barua ya Paulo kwa Wagalatia 5:16, anasema hivi: "Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili." K atika muktadha huu, Paulo anatuhimiza Waamini kuishi maisha yanayoongozwa na Roho Mtakatifu badala ya kushughulikia na kuridhisha tamaa za mwili. Katika maandiko ya Paulo,   "Roho"  inamaanisha Roho Mtakatifu ambaye anakuja kuishi ndani yetu wakati tunapo pokea wokovu kwa imani katika Kristo. Kuishi kwa Roho kunahusisha kuwa na uhusiano mzuri na Mungu kupitia kuunganika na Roho Mtakatifu. Kuongozwa na Roho Mtakatifu kunamaanisha kufuata mwongozo wa Mungu, kudumisha tabia na matendo yanayoambatana na ukweli na haki, na kuepuka kutenda tamaa za mwili ambazo haziendani na mapenzi ya Mungu. Wagalatia 5:22-23: "Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakun...

KUAZIMU AU KUKUSUDIA

  KUAZIMU MOYONI DANIELI 1:8 Katika kitabu cha Danieli katika Biblia, tunasoma jinsi Danieli na wenzake walikataa kula chakula cha mfalme Nebukadreza. Walifanya hivyo kwa sababu walitaka kushikamana na Sheria ya Mungu, na kujitenga na unajisi ambayo ilikuwa inaweka masharti ya chakula. Kulingana na Danieli 1:5-8, Nebukadreza alikuwa ameamuru kuwa watu waliochaguliwa kutoka kati ya wana wa Israeli walelewe na kuletwa kwenye jumba lake la kifalme. Mpango huo ulihusisha kuwapa chakula na divai kutoka kwenye meza ya mfalme mwenyewe. Hata hivyo, chakula hicho kilikuwa ni kinyume na Sheria ya Kiyahudi, kwani kilikuwa kimeandaliwa kwa namna ambayo haikufuata kanuni za kisheria. Danieli alikuwa mshikamanifu kwa Mungu na alijuwa Mungu ataka nini na kujitolea kwa sheria zake. Alihofia kwamba kula chakula hicho kingekuwa uvunjaji   wa amri za Mungu na kujichafua Kwa hiyo, aliamua  jaribio la kula chakula cha mboga na kunywa maji badala ya kula chakula kilichopangwa na mfalme. Jaribi...

UTU WA NDANI NA UTU WA NJE

    UTU WA NDANI NA UTU WA NJE

Nia,kiu na njaa ya haki ya Mungu

UINJILISTI 1).Mtu anayejua nia ya Mungu,mapenzi ya Mungu (Mt13:48; 1kor 1:21) Kazi ambayo Mungu anaithibitisha na kuitamani  Biblia ina fundisho lenye umuhimu mkubwa kuhusu uinjilisti, ambayo ni kazi ya kueneza na kushiriki Habari Njema ya wokovu kupitia Yesu Kristo na kuwaalika watu wamwamini. Yesu mwenyewe alitoa amri ya kwenda ulimwenguni kote na kuhubiri Injili.  Katika>>>) Mathayo 28:19-20, anasema, "Basi, enendeni, mkafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi. Na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. ” Hii ni agizo la moja kwa moja kutoka kwa Yesu kwa wafuasi wake kuhubiri na kueneza Injili. Katika Matendo ya Mitume, tunasoma juu ya juhudi za mitume na wafuasi wengine wa Yesu kuhubiri na kuwaleta watu kwa imani. Matendo 1:8 inasema, “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu ka...